THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY TIGO THE LEADING MOBILE COMPANY IN TANZANIA THAT VALUE AND LISTEN ITS CUSTOMERS. | AND NDOVU SPECIAL MALT "THE SMART CHOICE" | Karibu katika hii blog, Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Ila nawaomba tuweze kujieshimu kila mmoja wetu kwa kutumia lugha zisizo na matusi. Akhasante.

 

Jul 2, 2008
oldskool bash yakaribia

Zikiwa zimebaki siku nne tu kabla ya oldskool bash la karne kutimbuka nyongo, na watu kumwagika toka kila pembe ya dunia kweli vijana wa wazamani hawajasahau kuruka nyoka.

globu hii ya jamii ikizungumza na mmoja wa waandaaji wa hili libeneke la oldskuli ya karne,amesema hii bash sio ya kukosa wala kuhadithiwa,ni mambo makubwa ambayo hayajawahi kutokea, fika utikise kichwa,urushe japo mikono na kujiachia achia ili mradi si fujo wala patashika bali ni burudani la oldskuli litakalo kuacha hoi. ukichoka sana kutakua na starehe ya macho mbele yako kama show za break dance,chacha,robot n.k.


Amesema kwamba madebe yataanzia ijumaa kuanzia saa 4 usiku mpaka majogoo adresi ni 1213 E Dublin Graville,Columbus,Oh 43229.


Vijana wote wazamani walio Bongo,Ulaya,Canada na hapa Marekani wamekubali mwaliko akiwemo mbunge wa nanihii mheshimiwa nanihii.


amesema hii bash itakua ya kwanza katika historia ya bash za wabongo ya uwakutanisha Watanzania wanao toka mabara tofauti.


ratiba yaonesha kwamba jumamosi mambo yataanzia uwanjani kwa nyama choma huku tukiangalia mpira wa miguu kati ya Simba na Yanga. ikumbukwe mara ya mwisho timu hizi zilipokutana Washington Dc,Simba ililala 5-2. Hivyo hii itakua nafasi nzuri kwa Simba kulipiza kisasi.kama uwezo upo wa kusakata kabumbu njoo na vifaa.


Usiku wa hiyo jumamosi kuanzia saa 3 mambo ni kwenye RED KAPETI ni kuruka kopo mpaka asubuhi jua chomoza,adresi ni The Gathering,847 E..11th Av,Columbus,Oh 43211.


mdau unakumbushwa USISAHAU MSWAKI ila dawa za meno zitatolewa bureee,masaladi na amerikani chips watakuwepo ndani ya ukumbi kwa supu na chapati za nguvu.


mwisho waandaaji hao wamesema Dj Boni Luv atafanya onyesho moja tu, hilo la oldskuli july 5 Columbus ohio,hataweza kufanya onyesho lingine kwani july 12 Dj Boni Luv atakua Denmak.


Unaambiwa usikose hii nafasi ya kukutana, kuona na kucheza muziki wa dj huyu mahili na maarufu Tanzania.


ONESHO NI MOJA TU KWA DJ BONI LUV OLDSKOOL BASH COLUMBUS OHIO JULY 5

 
© Michuzi Tarehe: 2.7.08 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako |


Maoni: 3


  • Tarehe July 02, 2008 1:39 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    TUMAINI(INDEPENDENT SCHOLAR) NITAKUPITIA ALHAMIS USIKU TUKAJIKUMBUSHE ENZI ZETU.
    JF WOTE VILE VIKAO VYETU KAMA KAWA.
    MWANAKIJIJI ......VENUE ZOTE NI WHEELCHAIR FRIENDLY.

     
  • Tarehe July 02, 2008 7:19 AM, Mtoa Maoni: Anonymous hatchet man

    hili bash,je litakuwa live bongo radio? na if yes,tunaomba starting time in GMT

     
  • Tarehe July 03, 2008 7:26 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    mimi niko mbali na marekani lakini nimeona mmeandika hii bash itakuwa live kwenye bongo radio. nataka sana kusikiliza show yote sasa ni saa ngapi show itaanza.

     


Idadi ya watu
eXTReMe Tracker